Isipite Wiki "Hamjapeana" na Mwenza WakoNajua wapo watakaoshangaa! Hee! Si mtachokana? Siyo kweli bwana, labda hampendani, kama kweli mnapendana msikubali wiki nzima ikakatika bila kupeana na Mkeo/Mumeo labda kuwe kuna sababu ya kueleweka mathalani ugonjwa, lakini isije ikawa "Ubize" na "Majukumu" mengine ndo chanzo cha kutopeana, Sasa Mmefunga ndoa ili iweje? Maana ndoa ni tendo la ndoa! Sasa kama nyinyi hamfanyi hilo tendo la ndoa lililowakutanisha kuna faida gani ya hiyo ndoa?!
                   Wapo ambao wameweka ratiba ya siku maalum za kufanya mapenzi na wenza wao mfano, usiku wa kuamkia jmosi na jpili, kwa kuhofia kutoharibu kazi na kutozisahau nyumba zao. Mimi nawaunga mkono kwanai pamoja na hayo, ikitokea dharura katikati ya wiki "Game" linapigika kama kawa! Hii itamfanya mwenza wako asijione mtumwa wa mapenzi na pia kumpa muda wa kupumzika kama shughuli yako ni nzito kidogo!
                     Tujitahidi kutokuwa na madeni ya mapenzi na wenza wetu kwani kufanya hivyo unafungua mianya kwa wezi kukuibia, ndo utaskia Mke wa Bosi anatembea na Dereva au Mlinzi, au Baba mwenye nyumba anatembea na Kabinti nje au hata House Girl wakati mwingine!! Tuwe Makini!!!!


Drop Your Comment Here


Related Posts


Previous
Next Post »