Kwanini Secretary wa Mumeo anajitegesha Kihivyo?Hivi wewe Mrs Boss fulani, ushawi jiuliza kwanini Secretari wa mumeo anijitegesha na kujirahisi kiasi hicho? kama ndiyo, umechukua hatua hatua gani? Ni Ukweli usiopingika kuwa wengi miongoni mwa mabosi hutembea na Masecretary wao, hasa wanapokuwa wana tofauti kidogo na wake zao. Sasa mama mwenye nyumba unachukua hatua gani? Kwanza Ondoa tofauti baina yako na mumeo. Pili Mweleze Ukweli Mumeo juu ya hofo yako kwa Mfanyakazi huyo. Tatu: Mueleze ni jinsi gani unampenda na utaumia kama atakuwa na mahusiano mengine na hasa kwa huyo unaye mhofia. Kwa upande mwingine Mwambie wazi huyo Secretary kama unahisi ana Mazingira ya kujirahi au kumtega Mumeo kwamba akae mbali na mumeo na achunge mavazi na vitendo vyake. Kikubwa zaidi tuwe na Tabia ya kuwatembelea Wenza wetu Katika Maofisi au Sehemu zao za kazi ili kujiwekea mazingira ya uaminifu na kuwavunja moyo wote wanaomkodolea macho kwamba mwenye mali yupo makini.


Drop Your Comment Here


Related Posts


Previous
Next Post »