Lini "Tufanye Mapenzi"?!!Habari za week end wapenzi wasomaji wangu! Ni matumaini yangu mpo salama na mnaenendelea vyema. Leo nataka kugusia kuhusu kufanya mapenzi, kwa vijana. Maamuzi yangu yanatokana na zama tulizonazo ambazo kiukweli maadili yameporomoka, na kila mtu analifanya lile alitakalo bila kujali Umri, nafasi, Mazingira au Jamii inayomzunguka.
        
    Kwa ambao wapo katika ndoa tayari najua hili si tatizo kwao, wamesalimika! Hapa nawalenga zaidi vijana, tena wale ambao hata miaka 20 hawajafika, vijana ambao kiukweli vichwa vyao vimekuwa vya moto mno, asilimia kubwa wanafikiria kuhusu "Ngono", Starehe na "Maisha ya gharama".
                   Katika Zama tulizonazo suala la Ngono na Mapenzi limekuwa la Uwazi Mno. Ki mtazamo wa kimaadili na imani, hatutakiwi kushiriki Mapenzi na Kujamiiana Mpaka tutapokuwa katika Ndoa, nami naliafiki na kulisimamia hili daima.
  Lakini katika jamii inayotuzunguka Ngono na Mapenzi si tatizo, muhimu ukumbuke kutumia "Condom" na uhakikishe au shiriki na mwanafunzi la sivyo utafungwa.
Ukirudi katika mitandao na sehemu nyingine pia Ngono na Mapenzi ni wewe tu na hela yako! Kama hela ipo basi utapata Ngono kwa kadri unavyojisikia.
             
 Hapa ndipo tulipofikia leo.Kwa Kijana, Mimi nakusihi ujiulize yafuatayo kabla haujaamua kuanza kushiriki Ngono na Mapenzi:-
i) Nimelazimishwa au napenda toka moyoni
ii) Madhara yanayoweza tokana na kitendo nachotarajia kukifanya nayafahamu?
iii) Mwili, Viungo na Akili yangu ipo tayari kwa hayo?
iv) Wazazi, Jamaa na Imani yangu inasemaje kuhusu hili? 
 Kama utaridhishwa na majibu binafsi toka kwako mwenyewe nna uhakika utatoa maamuzi ya busara kuhusu lile ulilokusudia kulifanya na hata kama litatokea lolote utajua ni nani wa kumlaumu.


Kama nilivyosema awali, si malengo ya Blog hii watu wawe mafanyaji ngono sana au wazinzi wakutupwa, dhamira ya Blog hii ni kuwapa Habari, Elimu na Changamoto zinazotukabili wanajamii tuliokuwa katika mahusiano na ndoa kwa ujumla .Hatutegemei kuwaona watoto wakikazana kuitembelea Blog hii, lakini kwa mazingira ya ukweli na uwazi tuliyonayo hatuwezi kuwazuia, ila tutawapa tahadhari kwa baadhi ya " Maelezo ya Humu" ambayo hayajawalenga wao, na kuwakumbusha kuhusu umuhimu wa wao kujiweka mbali na masuala ya ngono na Mapenzi mpaka watakapofikia umri unaoruhusu na kama Imani zetu Zinavyotuambia.


Drop Your Comment Here


Related Posts


Previous
Next Post »