Mke Zungumza na MumeoKweli wanawake mnatakiwa kuwaheshimu na kuwatii waume zenu, na miongoni mwenu mnakuwa na utii wa kupitiliza ambao huambatana na aibu. Aibu hii hasa huja mnapotaka kuongea au kujihusisha na masuala ya mapenzi! Aibu na utii huu ambao sidhani hata kama Mungu anauridhia hupelekea "kuvumilia" adha ambazo kiukweli hazikutakiwa kuendelea kuwepo kama mke angakaa na mumewe na kumueleza.
Miongoni mwa matatizo wanayokumbana nayo wanawake ni pale mume anapokuwa hana subira na kuwa na papara katika kufanya mapenzi, hii humfanya mke kutofurahia "Raha ya Tunda" na mbaya zaidi kuumia kabisa, kuna baadhi ya wanawake wanahisi kumwambia mumewe vipi amuingilie au wafanyaje ili wote wafaidi raha ya penzi ni kitendo cha uhuni! hapani si kweli.

Waondoe uwoga huo na kujaribu kukaa faragha na waume zao na watoe maduku duku ya moyoni kwani huenda mumeo akawa anafanya jambo la kukuudhi au kukuumiza  bila kukusudia au hajui linafanyika vipi.Hivyo ipo haja ya Mke Kufunguka na kusema na Mumeo!!


Drop Your Comment Here


Related Posts


Previous
Next Post »