Mpe Unyumba Bila Masharti.
Naomba nizungumzie kidogo kuhusu hili, kuna baadhi ya wanawake tena wapo ndani ya ndoa, wanawawekea masharti waume zao katika suala la unyumba, kweli! Kwanini ulikubali kuolewa ikiwa kilichawaleta pamoja hutaki kukipa kipaumbele kinachostahili. Nayasema haya sababu, leo nilikaa na mtu wangu wa karibu, akiniambia eti mama Enjo, huwa na kwaida ya kudai hela za matumizi mbali mbali kabla ya unyumba na ikitokea baba Enjo hana kiasi kilichotajwa basi ndo imekula kwake na mambo hapewi. Tusiwe wanawake, ni wazi mumeo akiwa na hamu nawe, huwa tayari kwa lolote ili akidhi haja yake lakini usimtengenezee mazingira ya kwenda nje. Kama makahaba nje hufanya hivyo je wewe unajitofautisha kiasi gani nao? Hata kama kuna jambo au mahitaji unadai toka kwa mumeo, ni bora ukamwomba mkiwa ndani ya mechi au anapomaliza na akiwa amekelalia au umemlalia, kuliko kumuuzia mumeo haki yake.


Drop Your Comment Here


Related Posts


Previous
Next Post »