Mume Kutembea na "House Girl" ni KujidhalilishaLeo nizungumzie kuhusu Tabia ya Baadhi ya Wanaume walio katika ndoa zao kutembea na wasichana wao wa kazi. Ingawa imekuwa ikionekana kama ka mchezo ka kawaida lakini kwa watu wenye maadili na jamii endelevu ni kitendo cha kujidhalilisha, mimi nasimama leo kulikemea hili kwanza, haijalishi hata kama mkeo ana mapungufu kiasi gani au amekukosea kiasi gani. Hawa ni wafanyakazi wetu si nyumba ndogo za dharula, tusifanye hivyo haileti picha nzuri. Cha kushangaza utakuta mume ana mke mzuri, msafi tu lakini bado unaende kutembea na House Girl, haujishangai mwenyewe?! Noma bwana leo iwe ndo mwanzo na mwisho sio tu kwa kumwogopa Mungu au kumweshimu Mkeo, pia kujiepusha na uwezekano wa kupata maradhi ya kila aina ikiwemo UKIMWI kwani huwezi jua huyo House girl zaidi ya wewe kuna njemba ngapi nje zinajipigia! tuwe makini, haipendezi!


Drop Your Comment Here


Related Posts


Previous
Next Post »