Pesa ni Zako, Heshima kwa Mumeo Ibaki Palepale!Habari wapenzi wasomaji wangu? Leo niwageukie wale wanamama wenye mapesa yao halafu wapo katika ndoa, mimi naomba niwakumbushe nafasi na uzito wa mume ni bora na unathamani zaidi ya hizo hela wanazo miliki. Tusiwapande kichwani waume zetu eti kwa sababu tuna pesa zaidi yao, Tunawalisha au Tunagharimia shughuli zote za majumbani kwetu, Ingawa mumeo anaweza asilalame kwa hili kwa kuhofia utamwacha na yeye atakufa njaa lakini kaa ukijua atatafuta penzi la kuheshimiwa na kuthaminiwa nje! Na akilipita ndo ule usemi "Heri Lawama kuliko fedhea" Utatimia. Tujichunge na Pesa zetu kwa waume zetu.


Drop Your Comment Here


Related Posts


Previous
Next Post »