Simu zisitugombanishe
Mawasiliano ni kitu muhimu sana kwetu, lakini tunapozitumia Vibaya Simu zetu zinaweza sababisha Mzozo hasa na wenza wetu. Tuusitengeneze Mazingira hatarishi ambayo yatabomoa mahusiano yetu na hasa Ndoa zetu. Kama umeolewa, kwanini unampa jamaa wa nje namba yako, halafu akianza kupiga simu usiku unakosa la kumwambia Mumeo. Na wewe mume hawa viruka njia wa nje wa nini, si tayari una wako? unamwomba namba ili iweje? Pumb*** kabisa! Ili kutengeneza na kurudisha mazingira ya kuaminiana ni vyema tukawa na Uhuru wa maingiliano ya simu, yaani Mpenzi wako awe huru kuigusa na kuitumia simu yako kwa kadri aonavyo sahihi. Sio mara simu ina SECURITY CODE, mara IPO SILENT wakati mpo pamoja, tuachane na mambo hayo na tutulie na wetu!


Drop Your Comment Here


Related Posts


Previous
Next Post »