"Tutakumbushia na Wangapi"?Habari za leo wapenzi wasomaji wangu? kwa uchache leo tujiulize, kila mtu amewahi kuwa na mahusiano hapo awali. Kuna wakina sisi mpaka leo tupo katika mahusiano ya muda mrefu tumeshapitia mahusiano na watu zaidi ya kumi tofauti tofauti. Imetokea umekutana na miongoni mwa wapenzi wako wa zamani, ambao bado mnaongea ua hamkuachana kwa ugomvi, naye akakuomba eti " Mkakumbushie" Inakuaje hapo?

Binafsi niseme kwamba maji yakisha mwagika hayozoleki, zaidi ya kuyafuta tu na kuanza upya, hivyo basi kwa zama hizi tulizonazo mambo ya "kukumbushia" jamani hayapo, tusije peana maradhi ya ajabu kwani huwezi jua mlipotengena ni njia zipi kila mmoja alipitia, pia haitaleta picha nzuri kwa mwenza wako wa sasa.
Sijui wale ambao tumepitia mahusiano ya zaidi ya watu 20, kama kukumbushia tutakumbushia na wangapi??!!

ADIOS!!!!!


Drop Your Comment Here


Related Posts


Previous
Next Post »