Tutoke na Wenza Wetu!!
              Habari za ukimya wa siku mbili wapenzi wasomaji wangu? Ni matumaini yangu wote ni wazima na mnaendelea vizuri na maandalizi ya shughuli za mwisho wa mwaka!!! Loh, nilisafiri na kwenda maeneo ya ndani huku, hata network haipo vizuri. Nlichokiona ni tabia ya baadhi ya wanaume wa huko kupenda kutoka na wanawake, lakini sio wake zao, wanaume hawa hupoteza gharama nyingi kwa kuligharamia penzi la siku moja ile hali wana wenza wao huko na hawapati matunda na huduma bora kama hizo!
                  Kuelekea msimu huu wa siku kuu na mwaka mwaka mpya natoa wito kwa wanaume na wanawake ambao wapo katika mapenzi na ndoa, wawe ni wenye kutoka na wenza wao na si vinginevyo! Mbali na kipindi hiki yafaa katika mwezi angalau kutoka na Mkeo/Mmeo, kwenda sehemu iwe ufukweni au sehemu iliyotulia, mkakae, na itapenza Mkakodi "Chumba" kabisa na mkalala huko huko ili mfaidi vizuri! Tusiwe wenye kutoka na Kuwacha wenza wetu majumbani!!!


Drop Your Comment Here


Related Posts


Previous
Next Post »