Tuyaenzi Mambo Matamu kabla ya Ndoa zetu
Sote ni mashahidi wa hili, kuwekuwa na vilio vingi hasa upande wa wanawake kwamba Mme wangu ameacha kunitoa Out tangu tulivyooana tofauti na kipindi tupo wachumba au tangu nilipozaa tu mapenzi yamehamia kwa mtoto na ya kufanana na hayo. Mimi leo nawakumbusha wanaume wenzangu hii ni sumu katika nyumba zetu, kama ilikuwa ni kkawaida kutoka japo mara moja kwa mwezi kipindi cha uchumba basi tujitahidi kipindi cha ndani ya ndoa tutoke japo twende sehemu tofauti na za kipindi kile , mfano kabla ya ndoa au kuzaa mlikuwa mnapenda kwenda CLUB au Viwanja vya kujirusha na mkacheza mpaka basi, basi si vibaya mkitoka japo mara moja kwa mwezi baada ya ndoa na kwenda japo kiwanja ambacho haitawalazimu kucheza saaana, ila mtafurahisha nafsi zenu na mtakuwa bado hamjapoteza Utamu na Mapenzi mlozoeshana. Hii pia inahusika hata Kitandani, maana kuna njemba huwa wafanyaji wazuri sana wa mapenzi kwa staili na mbwembwe tofauti kabla ya kuoana, lakini ukishamuoa tu unakuwa mchovu, spidi inakata, tusifanye hivyoooo!


Drop Your Comment Here


Related Posts


Previous
Next Post »