Ukihisi Unasalitiwa, Chunguza Kimya Kimya!
Itakuwa haina maana kama unamfatilia ua kumchunguza mwizi wako, ile hali mwenyewe anajijua anafatiliwa. Huenda ikatokea unamuhisi mwenzio anatoka nje ya ndoa, basi usianze kumtolea maneno makali au kumtukana kumbe ni hisia tu au maneno ya watu wenye nia mbaya na ndoa yenu, kama itabidi utafute au ushirikisha watu wa nje wakusaidie katika uchunguzi wako ili kujihakikishia mambo yapo vile unavyofikiri au la! Wakati uchunguzi ukiendelea nyie hasa hasa wewe endelea na mapenzi kwa mwenzio kwa kiwango cha hali ya juu zaidi na usioneshe dalili za kumtilia mashaka au unamchunguza kwa namna yoyote ile, hii itasaidia kuujenga uhusiano wenu baada ya utafiti wako kukamilika na ukaja kuujua ukweli wa mambo.


Drop Your Comment Here


Related Posts


Previous
Next Post »