Usafi Muhimu Katika Mapenzi
Pengine hili linawagusa wanandoa wengi pale wanapokutana Uwanjani, na wengi wetu tumekuwa wakimya na kuamua kuvumiliana ingawa linatukereketa moyoni. "USAFI" ni jambo muhimu sana katika kujihakikishia tunafurahia mapenzi na kupenda kufanya mara kwa mara na wapenzi wetu. Usafi wa Mwili na mazingira tupoenda kukutania, iwe chumbani au Sebuleni. kuhusu usafi wa mazingira, haunipi shida sana, tatizo ni usafi wa mwili, hapa napenda kusema kwa pande zote mbili kwa mume na kwa mke. Tusiruhusu harufu za ajabu ajabu ziharibu starehe yetu tuliorithishwa na Adam na Hawa, Harufu zinaweza zikawa ni za Kikwapa, Nywele za kichwani na mbaya zaidi ni harufu toka sehemu za siri. Tujitahidi kuoga kabla hatujakutana na wenza wetu, tusafishe sehemu zote ambazo tunahisi zina tabia ya kutoa harufu, tunyoe nywele za kwenye makwapa na sehemu za siri kwani nazo zinachangia kuleta harufu na mba wakati mwingine. Tujitahidi kupaka mafuta au manukato mazuri yasiyo na tabia ya kubadilika pindi tunapokuwa katika shughuli na kupoteza ladha ya mchezo, na la mwisho mawazo yetu tuyaweke mchezoni ili tuene raha ya mechi...........


Drop Your Comment Here


Related Posts


Previous
Next Post »