Zama Hizi "Wapendanao" Hatupigani!                  Naomba nichukue nafasi hii kusherehesha kidogo, maana kwa huku uswaz hapaishi vituko! Mara wanandoa hawa wamepigana, mara huyu kamfumania mumewe kapigwa! Loh! Kaazi kweli kweli! Mimi naomba niwape tahadhari wanaume au wanawake wenye mikono mwepesi ya kuwapiga Wenza wao, hayo ni mambo ya kizamani, kizazi hiki hiki cha kileo, hatutegemei tamaduni kama hizo kuendelea kuwepo!

                     Mbali na zama kutoruhusu, siku hizi kila mtu ana Ubovu wake kwa ndani na inawezakana hata mwenyewe hajijui, sasa wewe unaponyanua gumi lako kumpiga na ikatokea bahati mbaya akazimia au kufa unatakuwa umejiweka katika nafasi gani? Kwa wale wenzangu na mimi ambao wana hasira za juu ni bora kuondoka kwa muda eneo ambalo Mke/Mume amekuudhi ili kupunguza hasira zako na kuepusha madhara ambayo yangeweza kujitokeza kama ungeendelea kubaki.
Kila la kheri kwetu soote!


Drop Your Comment Here


Related Posts


Previous
Next Post »