Zawadi kwa "Mpenzi"Ni jambo ambalo watu wengi hasa wanandoa hawalipi kipaumbele chake. Lakini tuelewe ni jambo kubwa hata kama mke/mume ana kazi na uwezo kiasi wa kuweza kununua "zawadi" hiyo uliyomletea! Leo utakuta baadhi ya wake wa mabosi zetu wanaingia katika mitego ya vijana baada ya kijana kumsifia ana umbo zuri kisha akamnunulia ka bikini kadesign ya ajabu kisha mke huyo huyo akaivaa na akasifiwa sana na mumewe ambaye kwa upumbavu wake watu watammegea mkewe!
                     Lakini nisikulaumu sana mzee mwenzngu, we angalia ni vitu gani vipo katika Fashion, angalau kila weekend ukiwa haupo busy sana na kazi chomoka mara moja ingia madukani umnunulie Mamsapu vitu vya ukweli na hasa vinavyomuhusu yeye moja kwa moja.
                       Hii inakuhusu wewe pia mama fulani, usikubali mumeo akanunua Underwear, sox au Vest, na vya kufanana na hivyo hata kama anuwezo kiasi gani, kama uchumi sio mzuri bana hata katika hela ya chakula na umnunulie mwenza wako zawadi bwana! Vitu kama Viatu, Sox, Saa, Hereni, Cheni, Vidani, Chupi, Perfume, lotion au mafuta na sabuni, ni miongoni mwa vitu vidogo vidogo lakini vitakuwa na uzito mkubwa vikitoka kwa mwenza, pia ni silaha ya kuumiza vikiletwa na hawara au mnyemeleaji!


Drop Your Comment Here


Related Posts


Previous
Next Post »