Si kila wakati simba akikosa nyama hula majani.Mhh, kitambo kidogo nimewapa mgongo wapenzi wasomaji wangu, hii inatokana na kubanwa na majukumu mengine ya ujenzi wa taifa hata hivyo kwa kuwa hii ni Hobby na napenda hiki nnachokifanya najaribu kutafuta upenyo kila ntapokuwa naweza japo niwasilimie.

Haya sasa, turudi katika kijiwe au jamvi letu na kuanza kupashana ya hapa na pale, leo niwashtue wenzangu na mie ambao "eti" kwa kisingizio cha kukosa au kutompata mwenza wa uhakika huishia kuranda randa na kuchovya kila bakuli lilokuwa mbele yake. Najua tupo na wengi wetu tumepitia katika nyakati hizo mpaka sas tuna mshukuru mungu tumesalimika, sasa kwa wale wenzangu na mie ambao bado, hebu tujaribu kutulia na kumuomba mungu atujaalie tupate wenza wa kudumu katika maisha haya na kuacha kuranda randa maana mwisho wa siku tutakuja kujutia, na mbaya zaidi majuto hayo yakikuta kipindi ambacho unahisi umetulia na una kila sababu ya mafanikio.

Please, let us be More than Careful with our Lives!!!!  ADIOS!!!


Drop Your Comment Here


Related Posts


Previous
Next Post »