SAKATA-DOKTA EVA CARNEIRO: JOSE MOURINHO ‘AOSHWA’ NA FA! Eva Carneiro and Jon Fearn


BOSI wa Chelsea Jose Mourinho hatasulubiwa na FA, Chama cha Soka England, baada ya kumsafisha kwamba hakutumia lugha chafu dhidi ya aliekuwa Daktari wa Timu yao Mwanama Eva Carneiro.
FA ilipitia Mikanda iliyohusisha tukio la Dokta Eva Carneiro kubatukiwa na Mourinho kwenye Mechi ya Agosti 8 waliyotoka 2-2 na Swansea City baada ya Mdau mmoja kuwasilisha kwao malalamiko kuwa Meneja huyo alitumia lugha chafu.
Mara baada ya Mechi hiyo  na Swansea, Dokta huyo aliondolewa kuihudumia Timu ya Kwanza ya Chelsea.
Katika Mechi hiyo, Dokta Carneiro na Tabibu wa Viungo Jon Fearn waliingia Uwanjani kumtibu Eden Hazard kwenye Dakika za Majeruhi wakati Chelsea ipo 2-2 na Swansea City huku wakiwa Mtu 10 baada ya mapema Kipa wao Thibaut Courtois kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu.
Kitendo hicho kilimkera Mourinho kwani Mchezaji akihudumiwa na Madokta basi huwajibika kutoka nje ya Uwanja na husubiri amri ya Refa kuingia tena huku Gemu ikiendelea na hilo liliiacha Chelsea iwe Mtu 9 kwa Dakika kadhaa.
Mourinho alimponda Dokta huyo na kumsema hajui mchezo unakwendaje.
Hivi sasa Dokta Eva Carneiro amebwaga manyanga kuwepo Chelsea licha ya kutakiwa kurudi kazini na sasa yuko mbioni kusaka Sheria katika mamlaka husika.


Drop Your Comment Here


Related Posts


Previous
Next Post »