VPL: MABINGWA YANGA WAZIDI KUPAA KILELENI, AZAM WAFUATIA, SIMBA NAO WAJIKONGOJA!
LIGI KUU VODACOM
MATOKEO:
Jumatano Septemba 30
African Sports 0 Mgambo 1
Azam FC 2 Coastal Union 0
Kagera Sugar 0 JKT Ruvu 0
Mtibwa Sugar 0 Yanga 2
Majimaji FC 1 Ndanda FC 1
Prisons 0 Mwadui FC 0
Simba 1 Stand United 0


MABINGWA wa Ligi Kuu Vodacom, VPL, ambao pia ni Vinara wake, Yanga, Leo wameshinda Ugenini huko Morogoro baada ya kuichapa Mtibwa Sugar Bao 2-0.
Hadi Mapumziko Gemu ilikuwa 0-0.VPL-STAND-SEP30
Kipindi cha Pili Yanga walipiga Bao 2 kupitia Malimi Busungu Dakika ta 53 na Donald Ngoma Dakika ya 89.
Nao Azam FC, wakicheza kwao Chamazi, waliichapa Coastal Union 2-0 kwa Bao za Kipindi cha Pili za Shomari Kapombe na Kipre Tchetche.
Kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, Simba iliitungua Stand United Bao 1-0 kwa Bao la Dakika ya 58 la Joseph Kimwaga.
Matokeo haya yanaifanya Yanga ibakie kileleni ikiwa na Pointi 15 kwa Mechi 5 sawa na Azam FC lakini wao wako juu kwa ubora wa Magoli na Timu zinazofuatia ni Simba na Mtibwa zote zikiwa na Pointi 12 kila mmoja.
VIKOSI:
Mtibwa Sugar: Said, Rodgers, Issa, Andrew, Mbonde, Nditi, Barnabas, Mzamiru, Seleman, Ibrahim, Kichuya
Yanga: Mustafa, Juma, Haji, Nadir, Yondani, Said, Busungu, Kamusoko, Tambwe, Ngoma, Telela

LIGI KUU VODACOM
RATIBA
Alhamisi Oktoba 1

Toto Africans v Mbeya City
Jumamosi Oktoba 3
Mgambo Shooting v Coastal Union
Majimaji FC v Mwadui FC
Toto Africans v JKT Ruvu
Jumapili Oktoba 4
Stand United v Mbeya City
Kagera Sugar v Tanzania Prisons


Drop Your Comment Here


Related Posts


Previous
Next Post »