WENGER AMEMALIZA VISINGIZIO, MTIMUENI, MLETENI KLOPP, ADAI MDAU!

WENGER-KISAGO-OLYMPIAKOSWADAU wa Arsenal wamekuja juu na kudai Meneja wao Arsene Wenger sasa ameishiwa visingizio na umefika wakati atimuliwe na nafasi yake kuchukuliwa Jurgen Klopp.
Mmoja wa waliodai hivyo ni Piers Morgan ambae ni Mwandishi na Mwendesha Kipindi cha TV ambae alikasirishwa na Jana kutandikwa 3-2 na Olympiakos ya Ugiriki katika Mechi ya Kundi lao la UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL.
Hiki ni kipigo cha pili kwa Arsenal katika Kundi lao baada ya kuchapwa 2-1 na Dinamo Zagreb huko Croatia.
Piers Morgan alisema: “Ulikuwa ni uchezaji mbovu katika Mechi za Ulaya ambao sijapata kuuona katika muda wake wote Wenger akiwa Arsenal.”
Aliongeza: “Tulicheza ovyo dhidi ya Timu iliyofungwa mara zote 12 ikicheza England na kufungwa Mabao 37-3. Lakini Jana wametubamiza!”
Morgan alilalamika: “Wenger Siku zote ana visingizio, mara Uwanja, mara Fedha, Bodi, Hali ya Hewa. Kila kitu ni visingizio lakini si yeye Wenger. Jana visingizio vimeisha. Ni yeye!”
Morgan amedai Kocha wa zamani wa Borussia Dortmund, Jurgen Klopp, ndio anafaa kumbadili Wenger.
UCL-GROUP-F
Mechi zinazofuata kwa Arsenal kwenye Kundi F la UCL ni Mechi mbili mfululizo dhidi ya Bayern Munich ambao wameshinda Mechi zao zote 2 kwa kuzibamiza 3-0 Olympiakos huko Ugiriki na 5-0 Dinamo Zagreb huko Munich.


Drop Your Comment Here


Related Posts


Previous
Next Post »